Quantcast
Channel: HABARI – JAMIIBLOG
Viewing all 639 articles
Browse latest View live

KINANA AWATAKA VIONGOZI WA DINI KUIKEMEA CUF KUWAITA MAKAFIRI WANAOHAMIA CCM

$
0
0

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman, akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Pujini wilayani Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
 
Katika mkutano huo, Kinana alitumia staili yake ya kuwakataza wananchi kumshangilia akiwataka wamsikilize vizuri maneno aliyokuwa akizungumza kuhusu utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ambapo alimsifia Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein kwa uchapakazi wake kwa kuwaletea maendeleo wananchi katika visiwa vya Pemba na Unguja.
 
Alisema wakati wa uongozi wake amejenga barabara nyingi za lami, miradi ya maji, Afya na elimu karibu kila kona ya visiwa vya Pemba na Unguja, lakini wakati anafanya mambo yote hayo wapinzani wakiwemo viongozi wa CUF na wafuasi wao wanajifanya hawayaoni maendeleo hayo.
 
Alisema Serikali YA ccm iliyo chini ya Rais Dk. Shein imepeleka umeme, miradi ya maji na barabara za lami hata katika Jimbo la Mtambwe alikozaliwa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad.
 
Kinana amelaani kitendo cha CUF kuwaita makafiri watu wotinginee wanaokihama hicho kwenda CCM na vyama vingine, ambapo ameomba viongozi wa dini kulikemea jambo hilo, akidai hakuna binadamu mwenye haki ya kumwita mwenzie kafiri isipokuwa Mungu.
 
Pia alikemea vikali tabia isiyo sahihi iliyozuka ya kuwatenga waliokuwa wana CUF na kuamua kujiunga na CCM na vyama vingine, akidai kila mtu ana haki ya kujiunga na chama chochote akipendacho.
 Wananchi wakishangilia wakati Kinana akiingia kuhutubia katika mkutano huo.
 Msafara wa Komredi Kinana ukikagua shamba la miti la Ushirika wa Hatugombani Kata ya Kilindi wilayani Chakechake. Katika shamba hilo ambalo Kinana alishiriki kupanda miti lilianzishwa kwa msaada wa TASAF. Zaidi ya miti 34,000 imependwa.
 Aliyekuwa Mwanachama wa CUF na kuhamia CCM, Gharib Bedui Hamisi akionesha kadi yake kabla ya kumkabidhi Komredi Kinana aliyemkabidhi kadi ya CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Pujini, Chakechake, Pemba. Hamis alielezea katika mkutano huo kuwa baada ya kutangaza kuhamia CCM AMATENGWA NA FAMILIA YAKE PAMOJA NA BAADHI YA MARAFIKI ZAKE.
 Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mwanajuma Majid Abdallah akishiriki kupanda miti katika shamba la Ushirika wa Hatugombani.
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Daud Ismail akishiriki kupanda mti katika shamba la Ushirika wa Hatugombani.
 .Mwanachama mwingine wa CU aliyehamia CCM, Said Abdalah Ibrahim akionesha kadi ya CUF kabla ya kumkabidhi Komredi Kinana ili apatiwe kadi ya CCM
 Kinana akishiriki ujenzi wa jengo la CCM tawi la Mchangani Jimbo la Wawi.Wilaya ya Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba.
 Wafuasi wa CCM wakimlaki Kinana huku wakiwa na picha za Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein
 Komredi Kinana akishirikiana na Mwenyekitri wa Chama cha ADC Chakechake, Mohamed Said Abdalah (kulia) na Mwenyekiti wa Chadema  Uwandani Kombo Ali Abdalah aliposhiriki ujenzi wa Ukumbi wa shule ya Sekondari ya Uwandani katika Jimbo la Wawi, Chakechake.
 Kinana na viongozi wengine wa chama na serikali wakiondoka baada ya kushiriki kupanda miti katika shamba la Ushirika la Hatugombani.
 Kinana akishiriki kuotesha miche ya mikarafuu  katika shamba la Kikundi cha Hatukosani Jimbo la Chakechake
 Sehemu ya miche ya karafuu ikiwa imeoteshwa katika bustani ya Kikundi cha Hatukosani katika Kata ya Chanjanjawili, Chakechake
 Sehemu ya Mji wa Chakechake, Makao Makuu ya Mkoa wa Kusini Pemba.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Pujini/
Komredi Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Pujini, Wilaya ya Chakechake, Pemba
 Kinana akipanda mti  akatika shamba la miti la Ushirika wa Hatugombani, Shaia ya Kilindi, Chakechake, Pemba.

Filed under: HABARI

MAKAMBA NA NDOTO YA VITUO VYA MICHEZO VYA KANDA

$
0
0

Mbunge wa Bumbuli na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Habari na Masoko ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambaye hivi karibuni pia ametangaza nia ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa January Makamba(Pichani juu)  hivi karibuni ameainisha adhma yake ya kuinua kiwango cha michezo nchini.

Azma hizo zimo katika  katika mazungumzo yake na Padre Privatus Karugendo ambayo yamechapishwa katika kitabu ambacho gazeti hili imekipata nakala yake ambapo ameainisha azma ya kujenga vitua vya michezo vya kanda vyenye hadhi ya kiolimpiki.

Kwenye kitabu hicho, Makamba amejibu swali kwamba kitu gani kifanyike ili Watanzania waweze kujivunia wanamichezo wao. Makamba alisema, “Inafedhehesha sana kuona kwamba asilimia 79 ya Watanzania walikuwa hawajazaliwa mara ya mwisho tumeshiriki katika fainali za kombe la mataifa ya Afrika.

Mwaka huo huo wa 1980 ndio mara ya kwanza na ya mwisho tuliweza kushinda medali za Olimpiki. Rafiki yangu Mzee Suleiman Nyambui na Mzee wetu Filbert Bayi ndio walitutoa kimasomaso kipindi kile. Ni muhimu kurekebisha hili.” 

Ni ukweli usiopingika kwamba Tanzania imekuwa kama kichwa cha mwendawazimu katika medani ya kimataifa huku tasnia ya michezo ikiendelea kugubikwa na migogoro isiyokwisha. Kutokana na migogoro hii, Tanzania inaendelea kupoteza matumaini ya kung’aa katika medani za kimataifa.

Katika mazungumzo hayo na Padre Karugendo, Makamba  alinukuliwa akisema, “Lazima tutambue kwamba maendeleo ya michezo yanatokana na vitu muhimu vitatu. Kwanza, ni lazima kuwepo na vipaji, bahati nzuri nchi yetu ina vipaji vya kutosha katika aina zote za michezo. Pili, ni miundombinu na mfumo wa kubaini na kuviendeleza vipaji hivyo, hii  bado ni changamoto . Tatu, ni utawala, uongozi, na uendeshaji wa tasnia ya michezo, hii pia ni changamoto. Hivi vitu vitatu ni lazima viwepo ili tuweze kupata mafanikio kwenye medani ya michezo.”

Kama mgombea wa kwanza kutangaza nia yake ya kugombea nafasi ya Urais katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu, Makamba anaungwa mkono na vijana wengi kutokana na kuendesha siasa zake kisasa, kibunifu na kuepuka malumbano ya jukwaani.

Katika mazungumzo hayo Makamba alielezea fikra zake alizonazo hasa hasa kwenye kuendeleza vipaji vya Watanzania ambapo alisema, “Ni lazima tuanzishe vituo vikubwa vya michezo au ‘sports academies’ kwenye kila kanda ya nchi yetu vyenye hadhi ya Kiolimpiki.” 

Makamba aliongeza  kwamba, “Kutakuwa na vituo sita vya aina hii katika nchi yetu ambavyo vitazungukwa na shule za msingi na sekondari za ‘boarding’. Vituo hivi vitakuwa na lengo la kukusanya wanafunzi wote kwenye kanda husika ambao wameonekana kuonyesha vipaji ambavyo vinapaswa kuendelezwa. Ukweli ni kwamba bila kuendeleza vipaji katika mazingira mazuri, basi tusahau kabisa kufanya vizuri kwenye michezo. Hili linaweza kufanywa kwa ushirikiano wa serikali na sekta binafsi”.

Mheshimiwa January Makamba anakuwa mgombea wa kwanza wa Urais kuweka bayana mipango yake ya Tanzania Mpya katika maandishi. Anaendelea kufunguka kwamba katika tasnia ya michezo ni muhimu sana kuwekeza katika watoto. Zaidi ya hapo, kila timu ya ligi kuu ni lazima iwe na akademi na TFF iendeshe ligi kuu ya timu za watoto.

“Tufikie wakati ambapo timu za taifa za miaka 10 ijayo ziwe zinaandaliwa kuanzia sasa, na serikali itenge bajeti kila mwaka kwa timu hizo  ili kuziwezesha kukaa kambini, kufanya mechi za majaribio na kuziwezesha kushiriki kikamilifu katika mashindano ya kimataifa. Mimi sio muumini wa hizi kamati za zimamoto kusaidia timu ishinde ghafla ghafla wakati siku zote watu hawafanyi maandalizi ya muda mrefu” alimalizia Makamba.

Makamba pia aligusia kuhusu suala la ukata na ufinyu wa bajeti unaokabili tasnia za michezo. Siku zote tunaona timu za taifa za olimpiki au jumuiya ya madola kukosa fedha za kukaa kambini ambapo huchangia katika matokeo hafifu.

“Huko nyuma, taasisi na mashirika ya umma yalikuwa na timu za michezo zilizokuwa zinafanya vizuri na kutoa michango kwenye maendeleo ya michezo. Kwa mfano, Pamba ya Mwanza, Sigara, Reli ya Morogoro, ushiriki huu ulichangamsha sana michezo na ni lazima turudishe utamaduni huu,” alimalizia Makamba. 


Filed under: HABARI

USAFIRISHAJI NA UCHUKUZI TANZANIA (CILT) KUFANYIKA MACHI, 3 JIJINI ARUSHA

$
0
0
 Balozi wa Heshima wa Taasisi ya Kimataifa ya Usafirishaji na Uchukuzi Tanzania (CILT), Waziri wa Jumuia ya Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe (kulia), akizungumza katika mkutano wa maandalizi ya kukusanya fedha kwa ajili ya mkutano wa kimataifa utakaofanyika jijini Arusha kuanzia Machi 4 hadi 5 ulioandaliwa na taasisi hiyo kwa ajili ya kuwajengea weredi wadau wa usafirishaji kutoka nchi mbalimbali duniani. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi kutoka Cilt, Zacharia Hans Poppe.
 Mwenyekiti wa CILT, George Makuke (kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Mipango wa MOT, Migire Gabriel, Balozi wa Heshima wa Taasisi ya Kimataifa ya Usafirishaji na Uchukuzi Tanzania (CILT), Waziri wa Jumuia ya Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi kutoka Cilt, Zacharia Hans Poppe.
Mkurugenzi wa Mipango wa MOT, Migire Gabriel, akizungumza katika mkutano huo.
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
 
Dotto Mwaibale
IMEELEZWA kuwa ukosefu wa weledi na utaalam wa masuala mbalimbali ya usafirishaji ndio chanzo cha kutokea kwa ajili nyingi nchini.
 
Hayo aliyasema jana Dar es Salaam Mwenyekiti wa Taasisi ya Kimataifa Usafirishaji na Uchukuzi nchini(FCILT), George Makuke wataki wakizungumzia maandalizi ya mkutano mkubwa unaotarajiwa kufanyika Machi mwaka huu Mkoani Arusha.
 
Mkutano huo utahusisha nchi mbalimbali Duniani ukiwa na lengo la kujenga weledi katika masuala ya usafirishaji na uchukuzi.
 
Akizungumzia mkutano huo alisema kuna mambo mengi yanafanyika katika usafirishai ambayo si sahihi hivyo mkutano huo utasaidia wahusika kutoa huduma kihalali.
 
“Ukiangalia kumekuwa na udanganyifu mkubwa katika masuala ya usafirishai kwa kuzidisha bei lakini hata watoa huduma wenyewe wamekuwa hawana weledi hivyo mkutano huo utajadili namna ya kuondia changamoto zote hizi”alisema 
 
Kwa Upande wa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe alisema kuwa mkutano huo ni mkubwa hivyo atahamasisha taasisi mbalimbali kutoa michango yao kwani unahitaji fedha nyingi kwaajili ya kuwahudumia wageni.
 
“Hasa nitaangalia namna gani taasisi za Wizara ya Maliasili na Utalii wamechangia kiasi gani maana wao ndio watakaofaidika kwani watu watatoka nchi mbalimbali hivyo itasaidia kuitangaza nchi”alisema 
 
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano huo,Zakaria Hans pope, alisema mkutano huo utasaidia kukuza uchumi kwani kama kukiwepo njia sahihi za usafirishaji mapato lazima yaongezeke. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

Filed under: HABARI

SAUTI ZA BUSARA WAMTAMBULISHA RASMI ALI KIBA

$
0
0
Msanii wa Bongo fleva nchini, Ali Kiba akiimba akapela moja ya nyimbo zake wakati wa mkutano huo na wandishi wa habari (Hawapo pichani), katika mkutano huo juu ya ushiriki wake kwenye tamasha hilo linalotarajia kufanyika Februari 12 hadi 15, Ngome Kongwe, Zanzibar. kushoto kwake, ni Mkurugenzi wa tamasha hilo, Yusuf Mahmoud ‘Dj Yusuf, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi wa Busara Promotions, Simai Mohammed.
**********
Mkali wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ali Kiba ametamba kukonga nyoyo watu mbalimbali watakaojitokeza kwenye tamasha la 12 la Sauti za Busara linalotarajia kufanyika, Februari 12 hadi 15, Ngome Kongwe, Zanzubar.
 
Ali Kiba alieleza hayo leo Alhamisi, Januari 29. wakati wa mkutano wa ulioandaliwa na Busara Promotions, wandaaji wa tamasha hilo kubwa la Kimataifa linalofanya muziki wa ‘Live’,  ambapo kwa mwaka huu zaidi ya wanamuziki na vikundi 37, watatoa burudani kwenye tamasha hilo kwenye viunga vya Ngome Kongwe, Unguja, Zanzibar.
 
Akizungumza mbele ya wandishi wa habari, Ali Kiba alisema kwa sasa amejiandaa kutoa burudani ya aina na ambayo itakonga nyoyo kwa watu wote watakaojitokeza kushuhudia tamasha hilo.
 
“Hii itakuwa ni zawadi kwa watanzania wote kunishuhudia nikiimba ‘live’ bila kutumia ‘cd’ kama wafanyavyo wengine. Mimi ni mwanamuziki na nimesoma muziki hivyo nitapiga muziki wa nguvu jukwaani” alisema Ali Kiba.
 
Na kuongeza kuwa, kwa sasa yupo kwenye mazoezi ya muda mrefu wa kujifua na bendi maalum  kwa ajili ya shoo hiyo huku akitamba kuwa, yeye ni msanii kwani muziki aliusomea na kujifunza huko nyuma alipokuwa  katika Nyumba ya kuibua vipaji THT, ambapo alijifunza vitu vingi ikiwemo kuimba muziki wa bendi na ‘live’.
 
Aidha, aliwaomba wapenzi na wadau wa muziki kujitokeza kwa wingikushuhudia tamasha hilo kwani wasanii mbalimbali wa ndani na nje watatoa burudani ya kipekee.
 
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa bodi ya Busara Promotion, wandaaji wa tamasha hilo, Simai Mohammed, alisema tamasha limeweza kuongeza ajira na uchumi wa Zanzibar kwani pia limeongeza fursa za utalii.
 
Kwa upande wake, Meneja wa tamasha  hilo, Journey Ramadhani, alisema tamasha hilo limeweza kuongeza fursa kila mwaka ikiwemo kutoa ajira kwa vijana wa kitanzania kwa asilimia 90, ambapo kwa mwaka huu wanatarajia kuwa na watendaji kazi na wa kujitolewa watakolipwa katika kusaidia tamasha hilo, zaidi ya watu 150.
 
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa tamasha hilo, Yusuf Mahmoud ‘Dj Yusuf’ alisema tamasha hilo limeweza kuibua wasanii mbalimbali ikiwemo kujitangaza kimataifa.
 
Aidha, Dj Yusuf alieleza kuwa, tamasha la mwaka huu litaendana na kauli mbiu ya kuimiza Amani, pia wameandaa tuzo maalum na zawadi maalum kwa wasanii wa Tanzania watakaoshinda katika kutunga nyimbo za amani.
 
Mbali na Ali Kiba, Wasanii wengine Isabel Novella kutoka  Msumbiji, Ihhashi Elimhlophe (Afrika Kusini),   Tcheka (Cape Verde),   Diabel Cissokho (Senegal),  Culture Musical Club (Zanzibar),  Msafiri Zawose (Tanzania),   Aline Frazão (Angola),   Tsiliva (Madagascar),   Leo Mkanyia and the Swahili Blues Band (Tanzania),   Mohamed Ilyas & Nyota Zameremeta (Zanzibar),   Thaïs Diarra (Senegal / Mali / Uswisi),   Liza Kamikazi and band (Rwanda),   Erik Aliana (Cameroon),  Mpamanga (Madagascar),   Mgodro Group (Zanzibar),   Rico Single & Swahili Vibes (Zanzibar),   Zee Town Sojaz (Zanzibar),   Ifa Band (Tanzania) na wengine wengi. Maelezo zaidi yanapatikana katika www.busaramusic.org
JAMII

Filed under: HABARI

AIRTEL YATOA MSAADA WA VITABU KWA SHULE YA SECONDARY NANJ MONDULI ARUSHA

$
0
0
Meneja Mauzo wa Airtel Kanda ya Kaskazini Brighthon Majwala akikabithi vitabu kwa Afisa Elimu wa shule za sekondari halimashauri ya Monduli Bwana Shaban Kasim Mgunya kwaajili ya shule ya sekondari Nanja iliyoko Monduli mkoani Arusha. wakishuhudia ni baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Nanja.
Meneja Mauzo wa Airtel Kanda ya Kaskazini Brighthon Majwala akikabithi vitabu kwa Afisa Elimu wa shule za sekondari halimashauri ya Monduli Bwana Shaban Kasim Mgunya kwaajili ya shule ya sekondari Nanja iliyoko Monduli mkoani Arusha wakishuhudia kulia ni Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde na kushoto ni mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Nanja Yona Lukas.
Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde akipitia kitabu na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Nanja mara baada ya Airtel kukabithi msaada wa vitabu vya sayansi kwa shule hiyo chini ya mpango wake wa Airtel shule yetu.
JAMII

Filed under: HABARI

WAFUASI 30 WA CHAMA CHA CUF WATINGA MAHAKAMANI HII LEO

$
0
0
Wanachama 30 wa Chama cha Wananchi CUF, leo wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam na kusomewa mashitaka matatu yanayo wakibili.
 
Washitakiwa hao waliofikishwa mbele ya Hakimu Mkazi, Emmilius Mchauru wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu walisomewa mashitako hayo matatu ambayo ni Kula njama ya kufanya jinai kesi inayowakabili watuhumuwa wote 30 kosa walilolitenda huko Temeke. 
Kosa la pili ni kufanya mkusanyiko usio halali na kosa la tatu ni kufanya mgomo wa katazo halali la Jeshi la Polisi ambapo kosa la pili na tatu linawakabili mtuhumiwa wa kwanza hadi 28.
Masharti ya dhamana yalikuwa wazi kwa watuhumiwa hao. 
 
 Ulinzi mkali wa polisi kwa watuhumiwa hao ambao walipelekwa rumande wakati mchakato wa dhamano yao ukifanyika ambao kila mmoja anatakiwa kusaini dhamana ya shilingi 100,000/= pamoja na mdhamini mmoja.
Ndugu na jamaa wakipata maelekezo kutoka kwa watuhumiwa hao.

Filed under: HABARI

WILAYA YA ARUSHA KUTENGEWA BILIONI 42

$
0
0

IMG_7036Mbunge wa Arumeru Magharibi Goodluck Ole Medeye akifafanua jambo katika kikao cha Baraza la madiwani kilichojadili bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha mjini kwa mwaka 2015/2016 ambapo kiasi cha shilingi bilioni 42.7 zimetengwa kusaidia upatikanaji wa huduma za maji,afya na elimu kama vipaumbele vikuu.Kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Arusha Fidelis Lumato,Mwenyekiti wa Halmashauri Saimon Saning`o na kaimu Mwenyekiti Anna Agatha Msuya.Kikao hicho kilifanyika jana katika ukumbi wa Halmashauri.(Habari picha na Ferdinand Shayo wa Jamiiblog)

IMG_7001

Mbunge wa Arumeru Magharibi Goodluck Ole Medeye akifafanua jambo katika kikao cha Baraza la madiwani kilichojadili bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha mjini kwa mwaka 2015/2016 ambapo kiasi cha shilingi bilioni 42.7 zimetengwa kusaidia upatikanaji wa huduma za maji,afya na elimu kama vipaumbele vikuu.Kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Mwenyekiti Anna Agatha Msuya. Kikao hicho kilifanyika jana katika ukumbi wa Halmashauri

IMG_7070Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Arusha Fidelis Lumato akielezea juu bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Arusha mjini kwa mwaka 2015/2016 ambapo kiasi cha shilingi bilioni 42.7 zimetengwa kusaidia upatikanaji wa huduma za maji,afya na elimu kama vipaumbele vikuu.Katikati ni  Mwenyekiti wa Halmashauri Saimon Saning`o na Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Mwenyekiti Anna Agatha Msuya. Kikao hicho kilifanyika jana katika ukumbi wa Halmashauri.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha vijijini ,Fidelis Lumato amesemakuwa wilaya yake imepanga bajeti ya kiasi cha shilingi bilioni 42  kwa mwaka wa fedha 2015 /2016 ambazo zitaelekezwa kwenye masuala ya maji,afya na elimu ili kuhakikisha upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii.

Fidelis Lumato aliyasema hayo jana katika kikao cha Halmashauri hiyo kilichojadili bajeti hiyo jana ambapo amefafanua kuwa mambo hayo matatu ni vipaumbele muhimu kwa halmashauri hiyo.Amesema kuwa fedha hizo zitasaidia kuboresha maabara,mabweni pamoja na kujenga vituo vya afya karibu.

Lumato amesema kuwa upatikanaji wa fedha hizo utasaidia ujenzi wa barabara ya Redio Habari Maalumu,Ngaramtoni,Seliani na Sambasha ambazo pia ni ahadi za Raisi Jakaya Mrisho kikwete.

Naye Mbunge wa Arumeru Magharibi Goodluck Ole Medeye amesema kuwa ni vyema halmashauri ikajikita zaidi kuboresha shule za msingi na sekondari  ikiwemo shule ya Sekondari Sokon 2 ambayo inakabiliwana uhaba wa matundu ya choo.

Medeye amewataka wananchi na madiwani kuwa wavumilivu baada ya mashimo ya nguzo  kuchimbwa kwenye maeneo yao bila kuwekewa umeme kwanimradi wa umeme vijijini  (REA) bado uko kwenye utekelezaji hadi utakapofikia kikomo juni 30 mwaka huu.

“Nawaomba madiwani na wananchi muwe wavumilivu badonafuatilia juu ya mradi wa REA bado wanaendelea na utekelezaji kwasasa kasi yaoinaenda kadiri wanavyopata fedha serikalini” Alisema Medeye

Diwani wa Kata ya Mwandeti Boniface Tarakwa amesemakuwa  bajeti hiyo ilenge kukarabati barabara ambazo hazipitiki hasa kipindi cha mvua ili kuboresha miundombinu .

JAMII


Filed under: HABARI

JAMII ISHIRIKI KUTATUA TATIZO LA WATOTO WA MITAANI

$
0
0
IMG_0342Shirika lisilo la kiserikali la The Foundation For Tomorrow linalojihusishwa na kutoa ufadhili wa masomo kwa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu na uboreshaji wa mfumo wa elimu Tanzania, lenye makazi yake jijini Arusha, limefanya mkutano wa siku mbili wa Tathmini ya shughuri zake kwa mwaka wa 2014 na kuwashirikisha washirika na wadau wa elimu kama vile mashirika na vituo vinavyojihusisha na huduma kwa yatima na watoto waishio katika mazingira magumu, Ofisi ya Afisa Elimu wilaya ya Meru, wakuu wa shule na vyombo vya habari. Mkutano huo uliofanyika mwishoni mwa wiki, ulikuwa na lengo la kuwashirikisha washirika wa shirika hilo majumuisho ya shughuri zake kwa mwaka 2014 na kuelezea mikakati yake kwa mwaka 2015 na kuendelea.
Meneja Uhusiano wa shirika la The Foundation For Tomorrow, Bw. Anton Asukile akielezea jambo wakati wa mkutano huo wa Tathmini ya Mwaka 2014.
Mmoja wa washiriki wa mkutano huo akichangia jambo.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakisikiliza kwa umakini kutoka kwa mmoja wa wachangiaji (hayupo pichani)
Mkurugenzi Mkuu (Tanzania) wa shirika la The Foundation For Tomorrow, Bw. Kennedy Oulu alielezea jambo wakati wa mkutano wa siku mbili wa Tathmini ya Mwaka 2014, ulioendeshwa na shirika hilo mwishoni mwa wiki jijini Arusha.


Mmoja wa washiriki wa mkutano huo akichangia jambo.
IMG_0304IMG_0312Meneja Uhusiano wa shirika lisilokuwa la kiserikali la The Foundation
of Tommorrow  Anton Asukile akifafanua jambo juu ya tatizo  la watoto
wa mitaani  katika mafunzo yaliyoandaliwa na taasisi hiyo.
IMG_0317Washiriki wa mafunzo yaliyoandaliwa na  taasisi hiyoshirika lisilokuwa
la kiserikali la The Foundation of Tommorrow juu ya namna ya
kukabilaina na tatizo la watoto wa mitaani

Jamii imetakiwa kushiriki katika kutatua tatizo la watoto wa mitaani linalozidi kuongezeka kila kukicha badala ya kukaa kimya na kuyaachia mashirika binafsi pamoja na serikali hali inayosababisha tatizo hilo kukua badala ya kupungua.

Hayo yamebainishwa na Meneja Uhusiano wa shirika lisilokuwa la kiserikali la The Foundation of Tommorrow  Anton Asukile amesema kuwa jamii imekuwa na mtizamo hasi juu ya watoto wa mitaani na kuwanyooshea vidole huku wakiwatelekeza bila kuchukua hatua jambo ambalo linasababisha tatizo hilo kukosa ukomo .

Anton ameeleza kuwa endapo tatizo la watoto wa mitaani halitatatuliwa linaweza kuwa tatizo kubwa kwa jamii pale ambapo watageuka na kuwa wahalifu,watumiaji wa madawa ya kulevya na  majambazi jamii haitasalimika hivyo ni vyema wakavalia njuga suala hilo.

“Mfululizo wa matukio ya uhalifu unaposikia habari za panya road ni hawa hawa watoto wa mitaani wanaungana na kufanya ujambazi na ukatili,jamii isifumbie macho suala hili na kuona kuwa hawahusiki kwani  madhara yake yatawakumba na kuwaathiri” Alisema Anton

Amezitaka familia kujenga uchumi imara utakaozisaidia familia zao kupata mahitaji hata inapotokea mzazi mmoja amefariki aliyebakia aweze kuhudumia familia watoto wasisambaratike mitaani kwa kukosa mahitaji muhimu.

Aton amezishauri  familia kutatua changamotozinazowakabili pamoja na migogoro inayowakabili ili kuepuka migongano inayopelekea wazazi kutengana na kuwaacha watoto bila msaada hali inayowapelekea kutimikia mitaani.

“Tatizo la watoto wa mitaani ni tatizo la jamii nzima lisipotatuliwa vyema linaweza kugeuka na kuwa janga la taifa hata sasa dalili zimeanza kujitokeza” Alisema Anton

JAMII BLOG FOOTER

Filed under: HABARI

SEKTA YA MADINI INAKABILIWA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI IKIWEMO UHABA WA WALIMU WA UKATAJI MADINI

$
0
0

SAM_0921 Mratibu wa kituo cha jimolojia Tanzania Bw.Musa Shanyangi akiongea na waandishi wa habari hivikaribuni kuhusu namna kituo hicho kinavyotoa mafunzo ya ukataji madini ya vito

SAM_0919Mwalimu msaidizi wa chuo hicho Bw.Jamal Dallos akiwa anaendelea na shughuli ya ukataji madini

SAM_0897Lilian Petro akikata madini kwaajili ya kutengeneza pete,mkufu ,jiwe hilo ni aina ya Quartz shape Oval

SAM_0898Grace Charles akiendelea na ukataji wa madini

SAM_0899Kulia ni Gladness John pamoja na Loveness Marteen wakiwa wanaendelea na shughuli ya ukataji

SAM_0900Magret Joseph akiwa anaangalia kwa makini namna alivyokuwa akikata jiwe kwa kutumia mashine maalum

SAM_0912Loveness Marteen anachukua fursa hiyo kuwataka wanawake wengine kujitokeza katika fani hiyo ya ukataji madini kwa kuwa hata wanawake wanaweza kufanya shughuli hizo kama wanaume

SAM_0917Aina mbalimbali ya madini kabla ya kukatwa

SAM_0918

Baada ya kukatwa na mashine muonekano huwa hivi

SAM_0908Wanafunzi wakiwa darasani wakiwa wanaendelea na shughuli ya ukataji madini

Sekta ya madini nchini bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa walimu na wataalamu wa kufundisha ukataji wa vito vya madini hali inayosababisha kuuzwa kwa madini ghafi nje ya nchi na kupelekea kuuzwa kwa bei ya chini na pesa nyingi kwenda nje
Hayo yameelezwa leo na mratibu wa kituo cha jimolojia Tanzania Bw.Musa Shanyangi wakati akiongea na waandishi wa habari katika kituo hicho kina kinachotoa mafunzo ya ukataji madini ya vito wakati wa mahojiano maalum na waandishi wahabari chuoni hapo ambapo wameanza kutoa mafunzo ngazi ya cheti kwa wahitimu 15 wakike ambapo chuo kipo katika halmashauri ya manispaa ya jiji la arusha.

Alieleza kuwa hivi sasa madini ghafi yanauzwa sana nje ya nchi kwa bei ya chini lakini kama wangeweza kuuza madini hayo yakiwa yameongezwa thaman na kuuzwa kwa bei ghali na kuwezesha fedha za kigen kubaki nchini na kuongeza pato la taifa .

Bw,Shanyangi aliongeza kuwa hivi sasa wameanza kuwafundisha kozi ya miezi 6 kwa wanafunzi 15 wakike ambapo wanafadhiliwa na Arusha women foundation fund iliyoko mjini ikiwa na lengo la kuwasaidia mabinti ili kuweza kusaidia sekta ya madini na kuweza kukabiliana na uhaba wa wataalamu wa ukataji madini nchini.
Hata hivyo kituo hicho kinatarajia kuongeza wanafunzi mpaka kufikia 60 ili kuweza kuongeza ufanisi na kuweza kuboresha sekta hiyo ya madini ili kuweza kuongeza wataalamu ,pia wanamkakati wa kuweza kusomesha walimu wazawa ili kuweza kukidhi nakuwa na walimu na kupunguza gharama za kuchukua mwalimu kutoka nje yanchi ambapo hivi sasa wamemuajiri raia kutoka Sri lanka hali ambayo wanatumia gharama kubwa kumlipa mtaalamu huyo toka nje ya nchi.

BwShanyangi aliwataka wadaumbalimbali nchini pamoja na wawekezaji wawekeze katikak kufundisha wataalamu wazawa ili kuweza kukidhi mahitaji ya wakataji na wataalamu nchini.

Kituo hicho kimegharimu zaidi ya shilingi billion 1.2na mashine mbalimbali za kituoni hapo zimegharimu zaidi ya milioni 450 za ukataji na kusafisha madini hayo
Kwa upande wake mwanafunzi katika chuo hicho Bi.Joice Patrick alisema kuwa kupitia mafunzo hayo ya ukataji wa madini na ung’arishaji itawasaidia katika swala zima la ajira huku akiwataka wanawake kuchangamkia fursa hiyo
“Ni fursa sasa kwa wanawake kujitokeza katika kazi hii na waione kama kazi zingine na si kuwaachia wanaume tu “alisema Joice

JAMII BLOG FOOTER


Filed under: HABARI

OLOLOSOKWANI WAPIGWA MSASA KUKITUMIA VYEMA KIJIJI CHA DIJITALI

$
0
0
DSC_0066
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akiendesha mjadala kwa wanakijiji wa Ololosokwan na vijiji vingine vinavyozunguka kijiji hicho,viongozi wa halmashauri, viongozi wa kimila, viongozi wa vijiji na wataalamu mbalimbali wa sekta ya afya, elimu na uchumi ikiwa ni maandalizi ya kuupokea mradi wa kijiji cha kidigitali Ololosokwani wilayani Ngorongoro mkoani Arusha.
DSC_0095
Afisa mipango ya Elimu wa Shirika la UNESCO, Bi. Jennifer Kotta (kulia) akiwa kwenye majadiliano na baadhi ya wanakijiji wa Ololosokwan kuhusiana na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu na nini kifanyike kuboresha sekta ya elimu kwa ujumla katika kijiji hicho na kuishirikisha halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro katika maandalizi ya kupokea mradi wa kijiji cha kidigitali.
DSC_0231
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akisaini mkataba wa kukabidhiwa ardhi iliyotolewa na serikali ya kijiji kwa ajili ya mradi wa kijiji cha kidigitali huku tukio hilo likishishudiwa na uongozi wa juu wa serikali ya kijiji, wataalam kutoka UNESCO na halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro pamoja na wanakijiji. SOMA ZAIDI: KIDEVU MATUKIO

Filed under: HABARI

WASHINDI WA NDOVU GOLDEN EXPERIENCE WAZURU HIFADHI ZA SELOUS

$
0
0
 Meneja wa Kambi ya Lake Manze akiwaelekeza jambo washindi wa program ya Ndovu Golden Experience  iliyokuwa ikiendeshwa na TBL kupitia bia yake ya Ndovu walipokwenda kujionea vivutio mbalimbali katika mbuga hiyo mwishoni mwa wiki.
 Baadhi ya washindi wa program ya Ndovu Golden Experience iliyokuwa ikiendeshwa na TBL kupitia bia yake ya Ndovu wakirejea jijini Dar es Salaam mara baada ya kuzulu katika hifadhi ya Selous kwa siku mbili mwishoni mwa wiki.
Wakiwa katika utalii

Filed under: HABARI

MBUNGE JOSHUA NASSAR AWAONGOZA WANANCHI KATIKA MAKABIDHIANO YA HEKARI 92 ZA SHAMBA LA MADIIRA ARUMERU

$
0
0
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru,Dastan Malya akiwa na watendaji wengine wa serikali katika ofisi ya mtendaji wa kata ya Siela Sing’isi wakati mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar alipofika kwa ajili ya kwenda kutembelea Shamba la Madiira.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari akitia saini katika kitabu cha wageni katika ofisi ya kata ya Seela Sing’isi alipotembelea katika kijiji hicho cha Sing’isi.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassar akiongozana na Diwani wa kata ya Mbunguni Paul Laizer maarufu kama Askofu (shoto) wakati alipowaongoza wakazi wa vijiji vya Sing’isi na Malala kwenda kuangalia shamba la Madiira ambalo hekari 92 zimetolewa kwa vijiji hivyo.
Wananchi wa vijiji vya Sing’isi na Malala wakitizama sehemu ya eneo la Shamba la Madiira lililotolewa kwa wananchi wa vijiji hivyo.
Mpima wa Halmashauri ya wilaya ya Meru ,Seveline Luambano akiwaonesha wananchi wa vijiji vya Sing’isi na Malala,mipaka pamoja na michoro ya ramani ya eneo la hekari 92 zilizotolewa kwa vijiji hivyo .zoezi hilo limeshuhudiwa na Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassar.
Wananchi wakiwa katika Shamba la Madiira kutizama mipaka ya eneo ambalo limetolewa kwao.
Sehemu ya Shamba la Madiira.
Mbunge Nassari akiwaongoza wananchi wa vijiji vya Sing’isi na Madiira wakitembelea shamaba la Madiira kutizama mipaka ya eneo la Hekari 92 lililotolewa kwao.
Mbunge Nassari akimsikiliza Mwenyekiti wa kijiji cha Sing’isi  Elishiria Kimoto akitoa maelezo ya kusitishwa kwa zoezi la kuoneshwa eneo hilo hadi pale Maofisa Ardhi wa Halamashauri hiyo watakapo weka mionundo mbuni ya barabara katika eneo hilo.
Mbunge Nasari akizungumza na wananchi wa vijiji hivyo mara baada ya kutembelea maeneo kadhaa ya eneo la Shamba la Madiira ambao aliwataka kusitisha kilimo ili kuruhusu maofisa Ardhi kupitishwa greda kwa ajili ya kuchonga barabara pamoja na mitaa katika eneo hilo.
Wananchi wakiwa katika kikao cha pamoja.
Na Dixon Busagaga wa Globu

Filed under: HABARI

JK AMTEUA HAULE BALOZI MPYA WA KENYA, BATILDA AHAMISHIWA TOKYO JAPAN

$
0
0
Balozi mpya wa Tanzania, Tokyo JAPAN, DK Batilda Salha Buriani.

Filed under: HABARI

WAKULIMA 7 WAKABIDHIWA MATREKTA LEO

$
0
0

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akikabidhi funguo za trekta kwa Mwalimu wa Shule ya msingi Kwadelo Bw. Hamza Haji, matrekta saba yalikabidhiwa leo kwa wakulima chini ya usimamizi wa Diwani wa Kwadelo Alhaji Omari Kariati.


 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akikabidhi funguo za trekta kwa Dk. Edmund Mndolwa ambaye ni Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa ikiwa sehemu ya matrekta saba yaliotolewa na Alhaji Omari Kariati Diwani wa Kwadelo.

 Moja ya matrekta waliokabidhiwa wakulima ,Alhaji Omari Kariati ameshatoa matrekta 100 mpaka leo tarehe 5 februari 2015.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi matrekta saba kwa wakulima yaliyotolewa na Diwani wa Kwadelo Alhaji Omari Kariati ambapo aliwataka viongozi kushiriki shughuli za wananchi 
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akijaribu kuendesha trekta mojawapo kati ya matrekta saba aliyokabidhi funguo kwa wakulima kutoka sehemu mbali mbali nchini, waliopanda trekta hilo kushoto ni Mjumbe wa NEC kutoka Wilaya ya Korogwe Vijijini Dk. Edmund Mndolwa na kulia ni Diwani wa Kwadelo Alhaji Omari Kariati.
 Mafundi wakiendelea kuunganisha matrekta ya Kariati ambayo yametolewa na Alhaji Omari Kariati.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisaini kitabu cha wageni kwenye ofisi ya Kariati inayoshughulika na matrekta ya kilimo Kinondoni Vijana Jijini Dar es salaam.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na MNEC wa Korogwe Vijijini Dk. Edmund Mndolwa (kushoto) kulia ni Diwani wa Kwadelo Alhaji Omari Kariati kwenye ofisi ya Kariati inayoshughulika na matrekta ya kilimo Kinondoni Vijana Jijini Dar es salaam.(Picha na Adam Mzee)

Filed under: HABARI

KIONGOZI WA KANISA LA WAADVENTIST WASABATO DUNIANI AWASILI TANZANIA

$
0
0
Kiongozi wa Kanisa la Waadventist Wasabato (SDA) duniani, Askofu Ted Wilson (wapili kushoto) akingalia mkewe Bi Nancy Wilson akivishwa kitenge na wamama wa SDA Tanzania  wakati wa mapokezi yao Nhini leo alipowasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julis Nyerere  (JNIA) Dar es Salaam  kuhudhuria sherehe za utume zinazofanyika Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana ambaye ndiye aliyeongoza mapokezi hayo kiserikali.
 Viongozi hao wakiangalia gwaride maalum.
 Kiongozi wa Kanisa la Waadventist Wasabato (SDA) duniani, Askofu Ted Wilson na  mkewe Bi Nancy Wilson wakivishwa skafu.
 Gwaride maalum kutoka shule ya Msingi Heritage ya Ukonga Banana, wakitoa salam ya utii.
 Askofu Ted Wilson akipiga picha ya gwaride hilo.
Gwaride likitoa heshima maalum kwa Kiongozi huyo ambaye hii ni mara yake ya pili kuzuru Tanzania ila alikiri mapokezi haya ni ya kipekee.
 Gwaride lilikuwa la kipekee 
Kiongozi wa Kanisa la Waadventist Wasabato (SDA) duniani, Askofu Ted Wilson akisema neno na watoto hao na baadae kuwaombea.
  Kiongozi wa Kanisa la Waadventist Wasabato (SDA) duniani, Askofu Ted Wilson na mkewe wakizungumza na waandishi wa habari. 
 DC Rugimbana akiongoza ugeni huo.
  Kiongozi wa Kanisa la Waadventist Wasabato (SDA) duniani, Askofu Ted Wilson akisikiliza nyimbo kutoka kwaya maalum ya umoja.
  Kiongozi wa Kanisa la Waadventist Wasabato (SDA) duniani, Askofu Ted Wilson akizungumza jambo na wanakwaya hao hii leo.
JAMII

Filed under: HABARI

WAZIRI SIMBA AMSIMIKA CHIKAWE KUWA MLEZI UWT NACHINGWEA

$
0
0

1

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba (kushoto) akimsimika kwa kumvalisha joho la ulezi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, mkoani Lindi, Mathias Chikawe, kuwa mlezi wa UWT katika wilaya yake ya Nachingwea. Sherehe hiyo iliyohudhuriwa na mamia ya wanachama wa UWT, ilifanyika katika Ukumbi wa NR mjini Nachingwea leo.

2

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba (kushoto) akimsimika kwa kumkabidhi fimbo ya ulezi baada ya kumvalisha joho, kofia na skafu, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, mkoani Lindi, Mathias Chikawe, kuwa mlezi wa UWT katika wilaya yake ya Nachingwea. Sherehe hiyo iliyohudhuriwa na mamia ya wanachama wa UWT, ilifanyika katika Ukumbi wa NR mjini Nachingwea leo. Wapili kulia ni Mkuu wa wilaya hiyo, Regina Chonjo, na wapili kushoto ni mwanachama wa UWT wilayani humo, ambaye pia ni Mke wa Waziri Chikawe, Profesa Amandina Lyamba.

4

Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo (kushoto), Mke wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe, Profesa Amandina Lyamba (kulia) wakilisakata rumba na wanachama wenzao wa Umoja wa Wanawake (UWT) wilayani humo baada ya Mbunge wao kusimikwa rasmi na Mwenyekiti wa UWT Taifa, ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, kuwa mlezi wa UWT katika wilaya yake ya Nachingwea. Sherehe hiyo iliyohudhuriwa na mamia ya wanachama wa UWT, ilifanyika katika Ukumbi wa NR mjini Nachingwea leo.

5

Mlezi wa Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya ya Nachingwea, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto), akipokea zawadi kutoka kwa mwakilishi wa UWT wilayani humo baada ya Waziri huyo kusimikwa na rasmi na Mwenyekiti UWT Taifa, ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba (kushoto kwa Chikawe), kuwa mlezi wa UWT wilayani humo. Sherehe hiyo iliyohudhuriwa na mamia ya wanachama wa UWT, ilifanyika katika Ukumbi wa NR mjini Nachingwea leo.

7

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba akizungumza kwa furaha wakati akitoa hotuba yake kwa wananchama wa UWT Wilaya ya Nachingwea baada ya kumsimika Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto) kuwa mlezi wa UWT wilayani humo. Sherehe hiyo iliyohudhuriwa na mamia ya wanachama wa UWT, ilifanyika katika Ukumbi wa NR mjini Nachingwea leo. Katika hotuba yake hiyo, Waziri Simba alimuomba Waziri Chikawe aendelee kuisaidia UWT wilayani humo kama alivyokuwa anafanya awali. Kulia ni Mwenyekiti wa UWT, Mkoa wa Lindi, Faudhia Chiwangu.

8

Mlezi wa Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya ya Nachingwea, ambaye pia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akiwashukuru wanachama wa UWT wilayani humo kwa kumchagua kuwa mlezi wa umoja wao katika sherehe ya kusimikwa kwake iliyofanyika mjini Nachingwea leo. Katika hotuba yake, Waziri Chikawe ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, aliwaomba wanachama hao kuwa na ushirikiano kwa kuijenga CCM, pamoja na kuhakikisha wanawahamasisha wananchi jimboni humo kujiandikisha katika daftari la wapiga kura ili kujiandaa kwa kuipigia kura Katiba iliyopendekezwa pamoja na Uchaguzi Mkuu ujao. Kulia ni Mwenyekiti UWT Taifa, ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba ambaye alimsimika mlezi huyo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Regina Chonjo.

9

Mlezi wa Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya ya Nachingwea, ambaye pia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia), Mwenyekiti UWT Taifa, ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba (katikati) na Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Nachingwea, Ng’ondomole Modesta Makota wakiwaaga mamia ya wanachama wa UWT wilayani humo (hawapo pichani) wakati walipokuwa wanatoka ukumbini. Waziri Chikawe alisimikwa na Waziri Simba ili awe mlezi wa umoja huo na kuhakikisha kuwa UWT wilayani humo inazidi kusonga mbele. Sherehe hiyo iliyohudhuriwa na mamia ya wanachama wa UWT, ilifanyika katika Ukumbi wa NR mjini Nachingwea leo.


Filed under: HABARI

NOEL OLE VAROYA CHADEMA ATANGAZA KUWANIA KITI CHA UBUNGE ARUSHA

$
0
0

NOEL PICKatika picha ni Noel Olevaroya akihutubia Maelfu ya wananchi katika moja ya harakati zake katika mkutano wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

Aliyewahi kuwa mwenyekiti wa vijana na mjumbe Wilaya ya Arusha kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)Noel Olevaroya (37) ametangaza rasmi kupeperusha bendera ya chama hicho kwa kuwania nafasi ya ubunge katika jimbo la Arusha mjini

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha Noel Olevaroya alisema kuwa nia yake ya kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo la Arusha ni msukumumo kutoka kwa Mungu baada ya kumaliza nafasi yake ya uwenyekiti wa vijana na mjumbe wilaya ya Arusha mwaka 2014

Alieleza kuwa msukumo huo ulikuwa ukimsumbua sana na ndipo aliamua kutii sauti ya Mungu kwa kutangaza kuwania nafasi hiyo ya kugombea kiti cha ubunge katika jimbo la Arusha mjini ambapo kwasasa jimbo hilo lipo mikononi mwa Godbless Lema

Aidha alisema kuwa Mbunge anafursa nzuri sana ya kusaidia wananchi hata kwa kupitia mfuko wa jimbo,mshahara hali ambayo itasaidia kuwainua wananchi na kupunguza umaskini

Alitoa wito kwa vijana wa Arusha kusikiliza sauti ya Mungu kwa kuwachagua viongozi bora wenye hofu ya Mungu kwa maslahi ya Nchi yetu

JAMII BLOG FOOTER


Filed under: HABARI

ANGALIA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE NA QT 2014 HAYA HAPA

MBOWE:TUTAHAKIKISHA KILA MWANANCHI AMEJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA MPIGA KURA LAKINI KWA UPANDE WA KATIBA MSIMAMO WETU KAMA UKAWA UKO PALE PALE WA KUTOSHIRIKI

$
0
0
Mwenyekiti wa Chadema Freman Mbowe akiwa anasoma utuba wakati wa ufunguzi wa mkutano wa viongozi wa  chama hicho wa kanda ya kaskazini unaofanyika leo katika  hotel ya new Arusha jijini hapa
viongizo wa chadema  akiwemo mwenyekiti wakiwa wanasali kwanza kabla ya mkutano wa viongozi wakanda ya kaskazini kuanza
 Naibu katibu mkuu wa Chadema Salum Mwalimu akiwa anaongea nawaandishi wahabari
 MWENYEKITI wa chama cha demokrasi na maendeleo Chadema Freeman Mbowe amesema kuwa  chama chao kimejipanga kuahakikisha kinahamasisha  kwa  nguvu zote wananchi weweze kwenda kujiandikisha katika  daftari la mpiga kura 
 
Alisemakuwa hii itaweza kumsaidia kila mwananchi  kuweza kupata haki yakumchagua kiongozi bora  anaemtaka  katika uchaguzi mkuu  ujao  wa kuwachagua viongozi wakuu ambao ni rais ,wabunge na madiwani.
Alisema kuwa pamoja ya kuwa tume wamekuwa wananchelewesha kufanyika kwa zoezi hili , wao wamejipanga kikamilifu na pindi ambapo zoezi hili litatangazwa  kuanza rasmi watajitaidi kwa njia yoyote kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kujiandikisha
Alisema kuwa kwa upande wa kupiga kura katiba wanaendelea na msimamo wao ambao walitangaza awali wa kutoshiriki katika mchakato wa kura ya maoni ya katiba  huku akisisitiza kuwa swala la kutoshiriki katika mchakato wakura za maoni auingiliani kabisa na  kuhamasisha wananchi kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura
Alimaliizia kwa kuwasihi wananchi wajitokeze kwa wingi  sana pindi pale ambapo watasikia zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la kudumu limewadia  ili waweze kupata haki yao ambayo itawaruhusu kuchgua kiongozi wanao wataka.
 

Filed under: HABARI

SHIRIKA LA EQUALITY FOR GROWTH (EfG) LA ZINDUA MRADI WA MSAADA WA KISHERIA KWA WAFANYABIASHARA SOKONI

$
0
0

Kaimu Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Lushoto, Dk.Hassan Shelukindo (katikati), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa  mradi wa msaada wa kisheria kwa wafanyabiashara sokoni na ofisi ya mradi huo wilayani Lushoto mkoani Tanga jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la  Equality for Growth (EfG), Jane Magigita na Katibu Tawala wa wilaya hiyo (DAS), Josephine Kisigila. Mradi huo unaendeshwa na EfG.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la  Equality for Growth (EfG), Jane Magigita akitoa hutuba fupi kwa mgeni rasmi.
  Kaimu Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Lushoto, Dk.Hassan Shelukindo akizungumza katika hafla hiyo.
 Baadhi ya wasaidizi wa kisheria waliopatiwa mafunzo hayo.
 Wanawake wa Wilaya ya Lushoto wakiwa kwenye sherehe hiyo ya uzinduzi wa mradi huo na ofisi.

Viongozi mbalimbali waliojumuika kwenye uzinduzi huo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la  Equality for Growth (EfG), Jane Magigita (mbele katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wasaidizi hao wa kisheria na maofisa wa EfG.
 Wanahabri kutoka vyombo mbalimbali waliokuwepo kwenye uzinduzi huo. Kutoka kushoto ni Shadrack (Channel 10), Nasra Abdallah (Tanzania Daima), Dotto Mwaibale (Jambo Leo na Mtandao wa www.habari za jamii.com na Sophia kutoka Televisheni ya Mlimani.
 Wanafunzi nao walijumuika kuona shughuli mbalimbali za uzinduzi huo hasa kikundi cha ngoma kilichokuwa kikitoa burudani.
 Kikundi cha ngoma kikitoa burudani.
 Zawadi zikitolewa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa EfG, Jane Magigita.
 Mkurugenzi Mtendaji wa EfG, Mary Magigita akiwa ameshika mkungu wa ndizi aliozawadiwa. Kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Lushoto, Josephine Kisigila.
 Kaimu Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Lushoto, Dk.Hassan Shelukindo (kushoto), akifurahi na  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la  Equality for Growth (EfG), Jane Magigita baada ya kukabidhiwa machapisho mbalimbali ya EfG.
Maofisa wa EfG, Eva (kushoto) na Samora wakiwa katika maandalizi ya uzinduzi huo “Chezea EfG wewe”
******
WAJASIRIAMALI wanawake wametakiwa kutumia mafunzo ya usimamizi wa sheria katika masoko waliyopata kwa kuwaelimisha wengine badala ya kukaa nyumbani bila ya kutoa elimu hiyo.
 
Mwito huo ulitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Lushoto Dk.Hassan Shelukindo wakati wa uzinduzi wa ofisi ya mradi wa msaada wa kisheria kwa wafanyabiashara sokoni na ofisi ya mradi huo wilayani humo  mkoani Tanga jana kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo Jumanne Shauri. 
 
 
“Ninyi Wanawake wa Lushoto mmepata bahati kubwa ya kuletewa mradi huu pamoja na mafunzo haya mliyopata nawaombeni nendeni mkayafanyie kazi katika maeneo yenu” alisema Dk. Shelukindo
 
Alisema elimu waliyoipata ya msaada wa kisheria ni muhimu sana kusaidia jamii katika masoko na itasaidia kupunguza unyanyasaji wa kijisinsia.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la  Equality for Growth (EfG), ambalo linaendesha mradi huo, Jane Magigita alisema lengo la mradi huo katika wilaya hiyo ni kuhamasisha na kulinda haki za wafanyabiashara iwanawake katika masoko kwa kuwapatia elimu ya sheria, biashara, elimu ya vicoba, elimu ya uongozi na usimamizi wa vikundi.
 
Alisema EfG ni shirika la pekee nchini linalotoa msaada wa kisheria kwa sekta isiyorasmi hivyo kuonesha ni kiasi gani sekta hiyo ilivyo sahulika.
 
Alisema EfG  inaendesha mradi huo katika masoko ya wilaya ya Lushoto pamoja na vikundi mbalimbali vya maendeleo na kuwa shirika hilo linawajibika kutoa mafunzo  ya siku 25 kwa wasaidizi 25 ambao watasambaza huduma sheria kwa jamii.
 
Alisema mafunzo hayo yanatolewa kwa awamu tano ambapo kila awamu yatakuwa yanafanyika kwa  takribani siku tano.
 
” Shirika linawajibika kutoa mafunzo mafunzo mbalimbali kwa wafanyabiashara ikiwa na lengo la kuinua hali za wanawake wafanyabiashara sokoni kupitia mafunzo ya biashara, uundwaji wa vikundi vya Vicoba, mafunzo mbalimbali kwa watendaji na viongozi wa Halmshauri ya wilaya ya Lushoto kwa lengo la kuboresha hali za wafanyabiashara sokoni” alisema Magigita.
 
Alisema mpaka sasa shirika hilo limefanikiwa kuwapatia mafunzo ya sheria ya siku tano wasaidizi wa sheria 25, wanaume 8 na wanawake 17 kutoka katika masoko na wengine kutoka katika vikundi vya maendeleo ndani ya Halmshauri ya Wilaya ya Lushoto.
 
Alisema pia wanakituo maalumu cha msaada wa sheria katika ofisi za EfG Lushoto ambapo wafanyabiashara mbalimbali wanaruhusiwa kupeleka matatizo yao ya kisheria kila siku za Jumatatu na Jumatano kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa 10 jioni.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

Filed under: HABARI
Viewing all 639 articles
Browse latest View live